welcome note


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, August 25, 2011

..event planner & organizers

Hizi ni kampuni au oganizesheni ambazo kazi zao kubwa ni kuwafanyia mipango jinsi  watu wanavyopenda sherehe zao ziwe kama vile wanavohitaji. sherehe hizi huwa ni aina zote kutegemea na hitaji la muhitaji.Kuanzia harusi, birthday, communion, send off, bag parties, anniversaries, get together, family day za makampuni na sherehe nyingine nyingi tu.
kupitia hizi party & event organizer, huwezesha saidia watu kupata kile wanakichohitaji kwa uwezo wao tena kwa uhakika na umaridadi zaid hata tukaifurahia siku ile. Aina ya sherehe unayoitaka, idadi ya watu, ukumbi, hadhi ya sherehe, na mengineyo mengi kulingana na mahitaji  ndo humfanya mhitaji wa huduma hii kupatiwa gharama za huduma hiyo na kulipia kwa kazi hiyo.


Kitu hiki kimekuwa kigeni miongoni mwetu kwani ni kitu kipya ambacho wengi miongoni mwetu hatukitumii kwa kuogopa gharama na vitu vingine kama hivyo huku tukiendelea tumia KAMATI, zile tulizoziona jana kupitia hapahapa. ukweli ni kwamba planners na organizers hawa husaidia mengi, kwanza na kubwa kabisa ni MUDA, haina haja ya wewe mhusika kuhangaika huku na kule, huku ukitumia GHARAMA nyingi na wakati mwingine isilete matokeo tuyatakayo na baadae tuanze laumiana tena kati yetu na hata kusababisha kuharibu jambo zima.


Watu hawa hufanya mengi sana ili kuweza fanikisha siku yako kuwa ya kipekee na muhimu kama vile ulivopenda wewe, kuanzia venue, entertainment, transport, saloon, catering service, na kwa wale wataaopenda kushauriwa au kuchaguliwa rangi gani kwa upade wa mavazi yatakayotumika siku hyo oganizesheni hizi huwezesha yote hayo.

me nadhani umefika muda sasa wanajamii wenzangu tutumie zaidi hizi event organizer, party organizer kwa ajili ya kuandaa sherehe zetu zote , kwani kama tunataka save
                            MUDA  na
                            GHARAMA  pia, hata
                            LAWAMA zisizo na msingi,


ifike wakati kamati zikae pembeni, watu waendelee na kazi za kujenga taifa wakati hawa event and party organizer wakiendelea kutuandalia sherehe zetu kama hivi.


 na mwisho wa siku tujumuike kwa kuweka shida chini kutupa mikono juu  na kushereheka kwa furaha pamoja kw staili hii....


hata hiiii pia si mbaya, haya kwa zile party a kiofisi hiviiii.......


na kivingine yaweza kuwa kwa mtindo huuuu.........


na nyingine nyingiiiiiiiiiiiiiiii..............

yap, kwa leo ni hayo tu jaman wanablog ya yeahh, me naomba sikia zaid toka kwako kutokana na hili swala la hizi event and party organisers

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...