welcome note


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, August 24, 2011

vikao vya sherehe

vikao vya sherehe hutokea pale ambapo kuna sherehe fulani tunaitarajia kufanyika muda fulani baadae, yaweza kuwa kikao cha harusi, send off, kitchen party, vipaimara, birthdays, uadhimishwaji wa miaka kadhaa ya ndoa (anivessaries) na sherehe nyingine nyingi tu miongoni mwa jamii zetu.

vikao hivi hujengwa na wanakamati ambao huusisha ndugu, jamaa wa karibu na marafiki zetu ambao tunawaamin wataweza fanikisha sherehe zetu kupitia vikao hivi. Michango hukusanywa, kutoka kwa wale wasio wanakamati lakin pia ni wajumuikaji nasi pia katika sherehe hizi. Pia wengine huamua kutumia kamati zijulikanazo mijini tu kuweza kaa na kupangilia sherehe hizo (imekuwa kama biashara sasa)
Sasa vikao hivi vimeibua mengi miaka ya karibuni, kwan wana kamati wamekuwa na tabia ya kugeuza mitaji kwa manufaayao binafsi  kiasi cha michango ile inayokusanywa  hata kusababisha sherehe kutokuwa vile kama tunavopenda iwe nzuri. Wengi yamewakuta haya lakin wanaishia lalamika tu badala ya kuwasaidia wenzao wanaofuata wenye sherehe kama  hizo za kwao

wakati wa vikao hivi huwa kuna tabia ya  kupata vinywaji kidogo walau kuweka makoo sawa, sasa kuna wanakamati wengine hapa ndo huwa wanaona mahali pa kupata unywaji utafikiri hakuna kesho tena mbaya zaidi kwa kutumia pesa zilezile za mchango, hii si sawa jaman, tena wala si haki jaman. kama ni kurekebisha makoo na vinywaji, walau iwe kidogo na c iwe fujo basi

Tunawashukuru sana wanakamati wetu kwa kazi zenu ila ombi langu kwako wewe mwana'blog na mwanajamii yetu hii, tafadhali tufanye yale haswa yahusuyo kamati za sherehe tunazoombwa na ndugu au marafiki zetu waliotuamini kwa hilo. Ebu tuyaepuke yafuatayo na mengineyo tafadhali:
 - matumizi mabaya ya michango
 - unywaji wa pombe kupita kiasi 
  
  lakini je kuna umuhimu wa kuwa na hizi kamati wakati wa sherehe zetu???


natumai mwana"blog una ya ku'share nasi hapa, wala usisite jaman, ebu tuhabarishe jaman maana natumai umewahi sikia na hata kufikwa na yanayofanywa na hawa wanakamati wetu wa hizi sherehe zetu.................................................karibu

1 comment:

  1. vikao vya siku izi... watu wanataka kupata mitaji ya biashara na kumalizia kujenga nyumba zao...watz tubadilike

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...