....hapo ikiwa inang'oa nanga kuelekea Pemba na Unguja.
meli hiyo ilizama hapo kati ya Pemba na Unguja, kama ramani inavyoonyesha.
Na asubuhi ya mnamo tarehe 10 September 2011 hivo ndo ilivokuwa baada ya kutokea kwa ajali hiyo ambayo imeacha majonzi na msiba mkubwa huu nchini kwetu. Wachache waliweza nusurika, wakati mamia wakizama na kufariki dunia. Asilimia kubwa ya waliozama ni wanawake na watoto ambao walishindwa jiokoa katika hili
Na mpaka saa hii meli hiyo imeshazama kwenda chini kwa urefu zaidi ya mita 400, wakati huo huo bado kuna iadi kubwa ya watu waliokuwa wamejifungia vyumbani, vyooni na bado hawajaokolewa.
Ombi letu kwa waokoaji wafanye jitihada hata waweze toa watu hao huko chini na wazikwe kwa heshima zote kama binadamu wengine pale mwisho wa safari ya maisha yao ukifika.
Mungu awape nguvu wale wote waliopoteza ndugu wazazi, watoto, ndugu, jamaa na marafiki pia.
My condolesence to you all
No comments:
Post a Comment